Dalili za Ugonjwa Sugu wa Kubanwa Njia ya Hewa.
Ugonjwa Sugu wa Kubanwa Njia ya Hewa huathiri watu wenye umri zaidi ya miaka 40, ambao wamevuta sigara kwa miaka zaidi 20. Kawaida yake ni kuwa unakua taratibu na baadhi ya watu wanaweza wasifahamu kuwa wana ugonjwa. Hujidhihirisha kwa:
- Kikohozi sugu chenye makohozi: Makohozi hutengenezwa mara kwa mara.
- Tatizo sugu la kukosa pumzi linaloendelea kuwa kubwa linalozidishwa na mazoezi na lisilo na vipindi vya unafuu.
- Kuchoka mwili.
- Maambukizi ya kifua yanayojitokeza mara kwa mara au mkamba.
MUHIMU: * Watu wenye ugonjwa sugu wa kubanwa njia ya hewa wanalazimika KUACHA kuvuta sigara. Hii ndiyo njia bora zaidi ya kupunguza uharibifu wa mapafu.
* Dawa inaweza kutumika kupanua njia ya hewa, kupunguza mwako wa mapafu au kutibu maambukizi yanayoweza kusababisha mwako.
* Watu walioathirika wanaweza kusaidiwa kwa:
- Kuepuka hewa ya baridi sana.
- Kuhakikisha hakuna anayevuta sigara nyumbani.
- Kupunguza uchafuzi wa hewa kwa kuondoa moshi wa mekoni na vitu vinavyoweza kuwasha/kukera.