Jinsi ya Kujikinga na Ugonjwa wa Shinikizo Kubwa la Damu.
Ili Kuepuka Ugonjwa wa Shinikizo Kubwa la Damu, yatupasa kuzingatia yafuatayo:
- Punguza msongo wa mawazo.
- Tenga muda wa kupumzika kimwili na kiakili.
- Fanya mazoezi mara kwa mara.
- Zingatia jitihada za kupunguza uzito wa mwili wa ziada.
- Zingatia ulaji sahihi kwa kula mboga na matunda zaidi. Punguza ulaji wa wanga, sukari na mafuta.
- Punguza matumizi ya vilevi. Acha uvutaji wa sigara na matumizi ya mihadarati.
- Punguza matumizi ya chumvi na vyakula vyenye asili ya chumvi nyingi.
- Acha matumizi ya vinywaji vyenye kafeini.
- Pima shinikizo la damu mara kwa mara.
- Muone daktari kwa ushauri mara kwa mara.
Madhara yanayotokana na Ugonjwa wa Shinikizo Kubwa la Damu.
Mgonjwa wa Shinikizo Kubwa la Damu asiyezingatia maelekezo ya kitaalam kuhusu mfumo wa maisha na tiba, anaweza kupata madhara yafuatayo:
- Kiharusi -kuziba au kupasuka kwa mshipa wa damu katika ubongo.
- Moyo kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
- Upofu wa ghafla.
- Ugonjwa wa moyo.
- Figo kushindwa kufanya kazi.
- Shambulio la moyo.
- Kisukari.
MUHIMU: Mgonjwa wa Shinikizo la Juu la Damu, anapaswa kuzingatia ushauri wa kitaalam kuhusu tiba.
Mgonjwa wa Shinikizo Kubwa la Damu, anapaswa kuhudhuria kliniki mara kwa mara kwa ajili ya uchunguzi na ushauri.