Elimu Kuhusu Ugonjwa wa Shambulio la Moyo.
Ugonjwa wa Shambulio la Moyo una Dalili zifuatazo:
- Kushindwa kupumua vizuri/ipasavyo.
- Maumivu makali ya kifua.
- Maumivu ya kifua yanaweza kusambaa hadi mgongoni, mkono wa kushoto na taya kwa upande wa kushoto.
- Kuhisi kichefuchefu.
- Kutokwa jasho jepesi na maumivu ya kichwa.
MUHIMU: Ugonjwa wa Shambulio la Moyo ni Dharula. Ukipata dalili hizo, tafadhali wahi Hospitali haraka.