Elimu Kuhusu Ugonjwa wa Saratani.
Kuna aina nyingi za Saratani. Baadhi hujidhihirisha mapema huku baadhi hukaa kwa muda mrefu bila kubainika.
Visababishi vya Saratani.
Baadhi ya visababishi vya saratani ni pamoja na:
- Kuvuta sigara- Saratani za mapafu, mdomo na tumbo.
- Kutumia vilevi kupita kiasi- Saratani ya ini.
- Ulaji wa vyakula vilivyotakaswa- Saratani ya utumbo mkubwa.
- Maambukizi ya virusi- Saratani za tishu za limfoidi, mlango wa kizazi, ini na tumbo.
- Tiba ya mionzi ya ioni- Saratani za tishu za limfoidi na damu (leukaemia).
- Kutoshughulisha mwili.
Kumbuka: Dalili za Saratani hutegemea mfumo husika.
Zifuatazo ni Dalili za Ujumla:
- Kupoteza ladha ya kula.
- Kupungua uzito.
- Kuchoka mwili.
- Maumivu ya viungo au maumivu ya fumbatio.
Dalili nyingine:
- Uvimbe usio wa kawaida (kwenye ngozi, matiti).
- Kutoka damu kusiko kwa kawaida na kunakojirudia (uke, mkojo, njia ya haja kubwa, makohozi, matapishi).
- Mabadiliko ya tabia ya kawaida ya uchengelele (matumbo).
- Choo cheusi.