Elimu Kuhusu Ugonjwa wa Kisukari.
Baadhi ya Dalili za Ugonjwa wa Kisukari ni kama ifuatavyo:
- Kupata haja ndogo mara kwa mara na kiu kupita kiasi.
- Kukauka mdomo na ngozi kuwasha.
- Kuishiwa nguvu na uchovu kupita kiasi.
- Kutoona vizuri.
- Maambukizi ya mara kwa mara katika njia ya mkojo.
- Vidonda kuchelewa kupona.
- Kupoteza fahamu/kuzimia.
- Kupata ganzi miguu na mikono.
- Kupata magonjwa ya ngozi hasa fangasi chini ya matiti na sehemu za siri. Pia kupata majipu mara kwa mara.
- Kupungua kwa hamu ya tendo la kujamiiana.
Madhara Yanayotokana na Ugonjwa wa Kisukari.
Mgonjwa wa Kisukari asiyezingatia Maelekezo ya Kitaalam ya Tiba, anaweza kupata Madhara yafuatayo:
- Shambulio la moyo.
- Kukatwa kidole au mguu.
- Kiharusi-kuziba au kupasuka mshipa wa damu katika ubongo.
- Figo kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
- Kupungua kwa hamu ya tendo la kujamiiana.
- Kupoteza fahamu/kuzimia.
- Shinikizo kubwa la damu.
- Upofu.
- Kupata maambukizi kiurahisi.
MUHIMU: Mgonjwa wa Kisukari anapaswa kuzingatia ushauri wa kitaalam kuhusu tiba.
Mgonjwa wa Kisukari anapaswa kuhudhuria kliniki mara kwa mara kwa ajili ya uchunguzi.